Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.
Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu?
Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.
Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.