Kisha Esta akamwita Hathaki, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa mfalme, aliyemwagiza amhudumu Esta, akamtuma kwa Mordekai, ili ajue mambo hayo, na maana yake ni nini.
Basi yule Hathaki akatoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanda wa mji ulipo mbele ya mlango wa mfalme.
Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai.
Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema,