Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.
Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.
Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.