Je! Sikio silo lijaribulo maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?
Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.
Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi.