Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.
Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.
Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.