Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.
Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.
Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.
Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.
Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu.
Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.
Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.
Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.