Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.
Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana.
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.
Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.