Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka. Akasema, Mbona umepita kwa nguvu wewe? Mambo ya nguvu na yakuandame. Kwa hiyo jina lake likaitwa Peresi.
Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.
Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli.
Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.
Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.
Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa Bwana katika mwanamke huyu.
Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni;
Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.
Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.
Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.
Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
Yeye alikuwa wa wana wa Peresi, mkuu wa maakida wote wa jeshi mwezi wa kwanza.
Tena wakakaa Yerusalemu wengine wa wana wa Yuda, na wengine wa wana wa Benyamini. Wa wana wa Yuda; Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, wa wana wa Peresi;
Wana wa Peresi wote waliokaa Yerusalemu walikuwa watu mia nne sitini na wanane, mashujaa.
Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.
PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;