Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,
walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;
Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.
Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.